Soma Biblia Kila Siku 9Mfano

Yaelekea huyu kijana hakukusudia kwenda kutafuta malaya. Alinaswa kama mnyama aingiaye kwenye mtego asioujua. Hata hivyo kosa lake liko wazi. Lilianza, si kule tu alipomsikiliza huyo malaya, bali aliposhika njia iendayo nyumbani mwake wakati giza lilipoanza kuingia (m.8-9:Akiishika njia iendayo nyumbani kwake, Wakati wa magharibi, wakati wa jioni, Usiku wa manane, gizani). Ni vigumu kujinasua kuliko kujiepusha na ushawishi wa shetani na dhambi. Twajua dhambi inatutamani, na ni rahisi kunaswa tusipokuwa makini. Ndivyo Mungu anavyosema katika Mwa 4:7,Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde). Basi, moyo wako usizielekee njia zake(m.25)! Rudia pia m.4-5: Mwambie hekima, Wewe ndiwe umbu langu; mwite ufahamu jamaa yako mwanamke. Wapate kukulinda na malaya, Na mgeni akubembelezaye kwa maneno yake.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 9 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu na kupata maelezo mafupi ya kukusaidia kuendelea kutafakari na kuelewa Neno la Mungu. Mpango huu unagusa zaidi Kumbukumbu la Torati, Warumi na Mithali
More
Tunapenda kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabolimo.or.tz
Mipangilio yanayo husiana

Soma Biblia Kila Siku 12

SOMA BIBLIA KILA SIKU 01/20

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Kusikia Kutoka Kwa Mungu Kila Asubuhi

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

Soma Biblia Kila Siku Julai 2021

Upendo Wa Bure

Soma Biblia Kila Siku 10

Soma Biblia Kila Siku Februari 2021
