Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Usijisumbue kwa LoloteMfano

Anxious For Nothing

SIKU 6 YA 7

Itakuwaje kama utamsifu Mungu hata katikati ya maumivu? Brian alipitia hofu ambayo iliketa dalili zilizoonekana kimwili pia. Lakini kutokana na uzoefu wake, aligundua kwamba bado ana mengi ya kumshukuru Mungu. Hii hapa hadithi yake 



Kwanza nilishughulika na hofu kubwa na wasiwasi miaka kadhaa iliyopita nikiwa naishi katika nchi ya ugeni katika nyakati za changamoto ya maisha. Nikiwa najaribu kujifunza lugha mpya, kuanzisha biashara, kuwa nuru ya Kristo mahali ambapo hakukuwa na kanisa kabisa, na kulea watoto mapacha wa mwaka mmoja, ilikuwa kana kwamba taratibu nashuka kwenye bonde la giza.



Baada ya kipindi cha miezi kadhaa, nilipata maumivu ya kifua, kichwa na maumivu mengine ambayo yalikuwa kama kichocheo cha hofu na wasiwasi tofauti na nilivyozoea. Mpaka wakati huu katika maisha yangu, sikupigana na hofu sana, na nikiwa muwazi, nilidiriki hata kujisifia mwenyewe kwamba ni jasiri. Lakini mara nikaanza kuzama katika hali mbaya zaidi--nikishawishika kwamba kuna jambo baya kwangu au jambo baya litatokea kwenye familia yangu.



Watu wanauliza kwamba yawezekana hofu yangu ni ya kimazingira, kimwili, au kiroho. Nikiwa nimetafakari hili kwa muda, ninashawishika kabisa kwamba jibu ni "ndiyo." Naamini kabisa kwamba mara nyingi kunaweza kuwa na vitu vingi vinachangia. Msongo wa mawazo una njia ya kuchochea kiasi kwamba hata wale wenye kiwango kikubwa cha uvumilivu wanasalimu amri kwa nguvu hiyo.



Pia, kama vizuizi vya kimwili au ugonjwa, wengine wetu tunapitia nyakati ambapo miili yetu inakosa uwiano. Na pia, adui wetu wa kiroho anaonekana kama anatafuta nafasi inapokuja kwenye suala la mashambulizi, akipiga sehemu ambazo sisi ni dhaifu. 



Katika changamoto ya Paulo ya kutokujisumbua kwa neno lolote katika Wafilipi 4:6-7, anatutaka siyo tuu kuomba bali na kushukuru. Yaliyomo katika maagizo ya Paulo siyo baada ya kupata ushindi au kupata muujiza. Ki ukweli, Paulo mwenyewe alikuwa anakabiliwa na hali mbaya sana. Alikuwa anawaandikia kanisa la Wafilipi akiwa gerezani akikabiliwa na mustakabali usiojulikana. Lakini bado, waraka wake unaonesha furaha yake na hali ya kufurahi.



Kwa hiyo katika ya maumivu yetu, tunaweza kusifu pia.



Siamini kama Paulo anatutaka kuonesha shukrani ya uongo. Nadhani Paulo anatupa changamoto kushukuru panapostahili shukrani, hata katikati ya hali yoyote ya kupambana tunayopitia.



Nimejikuta kwamba sikosi vitu vya kusherehekea. Hata wakati wa nyakati za majaribu makali nayokabiliana nayo, kumekuwa na vitu vya kushukuru. Ukitafakari katika hivyo na kumshukuru husaidia kubadili mtizamo wangu na kufanya upya nia yangu.



Kujawa na mawazo hasi au mawazo ya msongo yanaweza kuleta mawazo ya hatari inayokuja. Lakini hata ninapoongelea shukrani zangu kwa Mungu kama tendo la nidhamu, mara nyingi naona uzito unaondoka. 



Hiyo haimaanishi kuna ucheshi fulani ili kupata maisha yasiyo na hofu. Lakini kanuni ya kumsifu Mungu hata katika maumivu ni njia inayoelekea katika uwepo wa mtoa uzima, unaotupa amani. 



-Brian


siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Anxious For Nothing

Ingekuwaje kama kungekuwa na njia bora ya kupigana na hofu isiyoisha inayokufanya kukosa usingizi? Pumziko halisi lipo--yawekana karibu zaidi ya unavyofikiria. Badilisha hofu na amani kupitia siku hizi 7 za mpango wa Bib...

More

Tungependa kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha