Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Usijisumbue kwa LoloteMfano

Anxious For Nothing

SIKU 1 YA 7

Kwa Kukimbia



Kuishi kwa hofu inaonekana kama unaishi kwa kukimbia--ingawa unayakimbia maisha yako mwenyewe. Hofu inajaa kifuani mwako unapojitahidi kwa bidii kukimbilia sehemu salama inayoonekana kama haifikiki. Mashaka yanazunguka kichwani mwako katika mwendo ambao inafanya vigumu kupumua, na hofu kuongezeka, na kusababisha kukosa uamuzi na mashaka. 



Yaonekana yakawaida? Kuna msukumo wa kudumu wa kutokufunga maisha yako--barua pepe hazisimami, taarifa nyingi zinajazana kwenye simu zetu, na tusisahau mtego wa kulinganisha unaoletwa na mitandao ya kijamii. Kwa hiyo, tunaishije navyo, wakati tunajua kama wafuasi wa Yesu, tumeitwa kuishi kutokusumbuka na lolote? 



Mara nyingi tunajisikia tumeshushwa na hukumu kwa sababu tunadhani Wakristo hawatakiwi kujisikia hivyo. 



Lakini itakuwaje kama tutaacha kukimbia vitu na tukaanza kumkimbilia mtu? 



Tunaweza. Unaweza. Ahadi a kwamba tunaweza kuishi kwa tusijisumbue kwa lolote haisimamii tunachoweza kufanya bali katika uwepo wa Mungu. Angalia inavyosema katika Wafilipi 4:6-7: SUV



“Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu.”



Sisi wenyewe, hatuna tumaini katika vita dhidi ya hofu. Lakini katika Mungu? Tuna njia kuingia katika uwepo wake, ambao unatoa amani ambayo hatuwezi hata kuanza kuuelewa.



Nini ni bora zaidi katika ahadi? Ni kitu cha kuendelea. Katika kila hali. Kila mara tunapoanza kusikia hofu, tunaweza kumwendea Mungu kwa ajili ya amani yake kwa sababu amani ni matunda ya uwepo wa Mungu. 



Hofu haiwezi kuondoka ghafla. Ni hatua kwa hatua, muendelezo wa kutafuta uwepo wake. Kwa siku chache zijazo, tutashirikiana hadithi za watu ambao kila siku wamepambana na hofu na walichojifunza katika safari hiyo.



Unataka kujifunza zaidi kuhusu maisha.Anxious for Nothing? Angalia Jumbe zinazofuana ili kupata amani zaidi. 



*kama unapambana na hofu, ni muhimu kutafuta msaada unaouhitaji. Kama unadhani una hofu, muone daktari wako. Kutafuta msaada hakukufanyi kuwa dhaifu, kunakufanya kwenye hekima.


siku 2

Kuhusu Mpango huu

Anxious For Nothing

Ingekuwaje kama kungekuwa na njia bora ya kupigana na hofu isiyoisha inayokufanya kukosa usingizi? Pumziko halisi lipo--yawekana karibu zaidi ya unavyofikiria. Badilisha hofu na amani kupitia siku hizi 7 za mpango wa Bib...

More

Tungependa kuwashukuru Life.Church kwa kutoa mpango huu. Kwa maelezo zaidi tembelea tuvuti ya https://www.life.church/

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha