Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 6Mfano

Soma Biblia Kila Siku 6

SIKU 28 YA 30

Maono ya mnyama wa nne ni ya kutisha kweli. Yanatupatia picha ya kuinuka na kuanguka kwa ufalme wa Shetani. Zile pembe ni mfano wa watawala wapinga Kristo watakaotekeleza mapenzi ya Shetani. Wa mwisho atapewa hata kuwashinda watakatifu wa Mungu (m.25: Watatiwa mikononi mwake kwa wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati). Nani atadumu? Tafakari Ufu 17:12-14: Zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama. Hawa wana shauri moja, nao wampa yule mnyama nguvu zao na mamlaka yao.Hawa watafanya vita na Mwana-Kondoo, na Mwana Kondoo atawashinda, kwa maana Yeye ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme, na hao walio pamoja naye ndio walioitwa, na wateule, na waaminifu. Mshindi ndiye Yesu. Kwa hiyo wote walio pamoja naye watashinda hata wakishindwa na huyo mnama, kwa sababu Yesu amewaita na kuwateua, nao wanaendelea kuwa waaminifu kwake hata katika kushindwa kwao.

siku 27siku 29

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 6

Soma Biblia Kila Siku 6 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha