Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 6Mfano

Soma Biblia Kila Siku 6

SIKU 10 YA 30

Mashindano kati ya Paulo na Barnaba yalimhusu Yohana Marko ambaye hakudumu pamoja nao hadi mwisho wa safari (m.38: Huyo aliwaacha huko Pamfilia, asiende nao kazini). Ulegevu huu ulimfanya Paulo aamue wasimchukue kwenye safari hii ya pili. Ila Barnaba alitaka wampe nafasi tena. Labda uamuzi wa Paulo ulikuwa mzuri zaidi ila Barnaba hakuweza kukubali kwa sababu Marko ni binamu yake (Kol 4:10 unasema mjomba,lakini tafsiri iliyo sawa ni "binamu"). Hata hivyo Bwana alizidi kuwatumia kwa kazi yake na baadaye walishirikiana tena vizuri. Hiyo inathibitishwa na 1 Kor 9:6, Je! Ni mimi peke yangu na Barnaba tusio na uwezo wa kutokufanya kazi?Na Kol 4:10, Aristarko, aliyefungwa pamoja nami, awasalimu; na Marko, mjomba wake Barnaba, ambaye mmepokea maagizo kwa habari yake; akifika kwenu mkaribisheni. Na 2 Tim 4:11,Umtwae Marko, umlete pamoja nawe, maana anifaa kwa utumishi.

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 6

Soma Biblia Kila Siku 6 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha