Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Maelezo ya mpango

Soma Biblia Kila Siku 6Mfano

Soma Biblia Kila Siku 6

SIKU 12 YA 30

Paulo alipotaka kuihubiri Injili Ulaya aliingia katika mapambano ya kiroho, lakini jina la Yesu ni jina la ushindi, ni jina kuu! Yule pepo wa uaguzi akamtoka saa ile ile(m.18)! Alikuwa amemsumbua Paulo siku nyingi. Bila shaka alikuwa ameliweka jambo hili mbele ya Bwana katika sala kama Yesu alivyofundisha: Yesu alipoingia nyumbani, wanafunzi wake wakamwuliza kwa faragha, Mbona sisi hatukuweza kumtoa?Akawaambia, Namna hii haiwezi kutoka kwa neno lo lote, isipokuwa kwa kuomba(Mk 9:28-29). Tukio hili liliwafanya Paulo na Sila kutupwa gerezani na kufungwa miguu kwa mkatale (mti uliochongwa na kutobolewa tundu kubwa). Je, hayo kweli ni ushindi wa Yesu au ni wa Shetani? Jibu litapatikana kesho!

siku 11siku 13

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 6

Soma Biblia Kila Siku 6 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.

Tungependa kushukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha