Hujaachwa: Kupata uhuru kama watoto wa Baba halisiMfano

Siku 3:
“Sikuweza kumsamehe baba yangu kwa sababu_____ .”
Je, umewahi kujisikia hivyo?
Kila uhusiano wa kibinadamu unatuhitaji kutoa na kupokea msamaha.
Haina tofauti na baba zetu wa duniani. Kuhusu msamaha ni kwamba tunaweza kuchagua kusamehe--au kuchagua kutokusamehe.
Inaweza kuonekana inatamanisha kutokusamehe wale waliotuumiza. Adui anatutega katika kufikiria kwamba kwa kutokumsamehe mtu, tunakuwaa na nguvu fulani dhidi yao. Lakini ukweli, tunaendelea kutoa yaliyopita--makosa waliyotutendea na watu walioyafanya, wana nguvu dhidi yetu.
Hebu fikiria hivi. Kila mara unaposema, " Sitamsamehe----------------," unaishi maisha ya maumivu na kuimarisha nafasi ya kutokusamehe kwenye kumbukumbu yako. Yesu hakufa kwa ajili yetu ili kuishi katika utumwa wa makosa ya zamani; alibeba kila kosa lililofanywa nasi na kwetu pia, ili tuishi kikamilifu na huru.
Msingi wa kuwasamehe waliotukosea, pamoja na baba zetu, ni kuangalia msalabani. Tukiwa na msalaba kwenye mtazamo wetu, tunatambua ukubwa wa dhambi zetu ulivyo, na jinsi ilivyomgharimu Mungu--uhai wa mwanawe!--kutusamehe. Tunapotambuka wingi wa msamaha tusiostahili tuliopokea, tunaanza kuona kwamba tunaweza kuwasamehe wote waliotukosea, pamoja na baba zetu.
Usinielewe vibaya. Msamaha haina maana kuhatarisha maisha yako kwa kudharau au kukana tabia ya matusi, na haimaanishi kufumbia macho dhambi. Mungu hakufanya hivyo kwetu. Bali, alitenda haki kwa makosa yetu kwa mwanawe asiyekuwa na hatia.
Hasira kamili ya kila kosa ambalo baba yako alikufanyia lilimwagwa juu ya Yesu msalabani.
Tunapoelewa hili, tnawekwa huru ili kuwasamehe baba zetu. Na kwa kuwasamehe, tunapata nafasi ya kutuma baraka ambazo hatujawahi kupokea kutoka kwa baba zetu wa duniani kurudi kwenye ukoo wetu. Kwa njia hii, tunaweza kuishi injili ya kupeleka neema kwa wasiostahili.
Pokea baraka za msamaha kutoka kwa Baba yako wa mbinguni. Toa baraka za msamaha kwa baba yako wa duniani, na tembea katika uhuru ukijua kwamba Baba yako wa mbinguni amekuahidi kukusamehe kila kosa na kukufuta kila chozi milele.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Louie Giglio, Mchungaji na Mwanzilishi wa Passion Movement, anashiriki nasi mpango huu wa siku 5 kuelewa sifa za Mungu katika kubadili maisha - kama baba kamili anayetaka utembee katika uhuru kama mtoto wake.
More