Soma Biblia Kila Siku 5Mfano

Wasiomwamini Yesu hakika hawataokolewa (Wakati wasemapo, Kuna amani na salama, ndipo uharibifu uwajiapo kwa ghafula; 5:3). Lakini si mpango wa Mungu kwao. Hakuwateua kwa ajili ya upotevu wa milele. Maana hakutuweka kwa hasira yake, bali tupate wokovu (m.9; ling. 1 Tim 2:4: Mungu Mwokozi wetu ... hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli). Twaweza kuwa na uhakika, maana Yesu alikufa kwa ajili yetu (m. 10; zingatia pia Rum 8:32: Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?). Katika m. 10 Paulo anabadilisha mfano. Maana ya "kulala" (m.10) si kulala usingizi wa kiroho kama katika 5:6f, bali "kulala mauti" (4:15). Yaani tuwe hai, tuwe tumekufa, Yesu akija, sote tutaishi pamoja naye milele. Tujengane katika tumaini hili!
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 5 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku pamoja na maelezo yatakayokusaidia kutafakari na kuelewa Neno la Mungu kwa urahisi.
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/
Mipangilio yanayo husiana

Soma Biblia Kila Siku 12

BibleProject | Safari ya Kujifunza Kutoka Luka Na Matendo

Soma Biblia Kila Siku 8

Soma Biblia Kila Siku Aprili 2021

Soma Biblia Kila Siku 9

Soma Biblia Kila Siku 11

Soma Biblia Kila Siku Machi 2021

Soma Biblia Kila Siku 10

Uamuzi Mkubwa Zaidi wa Maisha Yako!
