Zaburi 36:6-7
Zaburi 36:6-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Uadilifu wako ni kama milima mikubwa, hukumu zako ni kama vilindi vya bahari. Wewe, ee Mwenyezi-Mungu, wawalinda wanadamu na wanyama Jinsi gani zilivyo bora fadhili zako! Wanadamu hukimbilia kivulini mwa mabawa yako.
Shirikisha
Soma Zaburi 36Zaburi 36:6-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Haki yako ni kama milima ya Mungu, Hukumu zako ni vilindi vikuu, Ee BWANA, unawalinda wanadamu na wanyama. Ee Mungu, jinsi zilivyo na thamani fadhili zako! Wanadamu huukimbilia uvuli wa mbawa zako.
Shirikisha
Soma Zaburi 36