Zaburi 134:1-3
Zaburi 134:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Njoni kumsifu Mwenyezi-Mungu enyi watumishi wake wote, enyi nyote mnaotumikia usiku nyumbani mwake. Inueni mikono kuelekea mahali patakatifu, na kumtukuza Mwenyezi-Mungu! Mwenyezi-Mungu awabariki kutoka Siyoni; yeye aliyeumba mbingu na dunia.
Zaburi 134:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Njoni, enyi watumishi wote wa BWANA, Mhimidini BWANA Ninyi mnaohudumu usiku Katika nyumba ya BWANA. Painulieni patakatifu mikono yenu, Na kumhimidi BWANA. BWANA akubariki toka Sayuni, Aliyeziumba mbingu na nchi.
Zaburi 134:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tazama, enyi watumishi wa BWANA, Mhimidini BWANA, nyote pia. Ninyi mnaosimama usiku Katika nyumba ya BWANA. Painulieni patakatifu mikono yenu, Na kumhimidi BWANA. BWANA akubariki toka Sayuni, Aliyezifanya mbingu na nchi.