Zaburi 119:97-104
Zaburi 119:97-104 Biblia Habari Njema (BHN)
Naipenda sana sheria yako! Naitafakari mchana kutwa! Amri yako iko nami daima, yanipa hekima kuliko maadui zangu. Ninaelewa kuliko waalimu wangu wote, kwa kuwa nayatafakari maamuzi yako. Nawapita wazee kwa busara yangu, kwa sababu nazishika kanuni zako. Najizuia nisifuate njia mbaya, nipate kulizingatia neno lako. Sikukiuka maagizo yako, maana wewe mwenyewe ulinifundisha. Maneno yako ni matamu sana kwangu; naam, ni matamu kuliko asali! Kwa kanuni zako napata hekima, kwa hiyo nachukia kila mwenendo mbaya.
Zaburi 119:97-104 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Sheria yako naipenda mno ajabu, Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa. Maagizo yako hunitia hekima kuliko adui zangu, Kwa maana ninayo sikuzote. Ninazo akili kuliko waalimu wangu wote, Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo. Ninao ufahamu kuliko wazee, Kwa kuwa nimeyashika mausia yako. Nimeiepusha miguu yangu na kila njia mbaya, Ili nilitii neno lako. Sikuziacha hukumu zako, Maana Wewe mwenyewe umenifundisha. Mausia yako ni matamu sana kwangu, Kupita asali kinywani mwangu. Kwa mausia yako najipatia ufahamu, Ndiyo maana naichukia kila njia ya uongo.
Zaburi 119:97-104 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Sheria yako naipenda mno ajabu, Ndiyo kutafakari kwangu mchana kutwa. Maagizo yako hunitia hekima kuliko adui zangu, Kwa maana ninayo sikuzote. Ninazo akili kuliko wakufunzi wangu wote, Maana shuhuda zako ndizo nizifikirizo. Ninao ufahamu kuliko wazee, Kwa kuwa nimeyashika mausia yako. Nimeiepusha miguu yangu na kila njia mbaya, Ili nilitii neno lako. Sikujiepusha na hukumu zako, Maana Wewe mwenyewe umenifundisha. Mausia yako ni matamu sana kwangu, Kupita asali kinywani mwangu. Kwa mausia yako najipatia ufahamu, Ndiyo maana naichukia kila njia ya uongo.
Zaburi 119:97-104 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu. Ninaitafakari mchana kutwa. Amri zako zimenipa hekima zaidi kuliko adui zangu, kwa kuwa nimezishika daima. Nina akili zaidi kuliko walimu wangu wote, kwa kuwa ninatafakari juu ya sheria zako. Nina ufahamu zaidi kuliko wazee, kwa kuwa ninayatii mausia yako. Nimezuia miguu yangu isiende kwenye kila njia mbaya, ili niweze kutii neno lako. Sijaziacha sheria zako, kwa kuwa umenifundisha wewe mwenyewe. Tazama jinsi maneno yako yalivyo matamu kwangu, matamu kuliko asali katika kinywa changu! Ninapata ufahamu kutoka mausia yako, kwa hiyo ninachukia kila njia ya upotovu.