Zaburi 119:78-80
Zaburi 119:78-80 Biblia Habari Njema (BHN)
Wenye kiburi waaibike kwa maana wamenifanyia hila, lakini mimi nitazitafakari kanuni zako. Wote wakuchao na waje kwangu, wapate kuyajua maamuzi yako. Moyo wangu na uzingatie masharti yako, nisije nikaaibishwa.
Zaburi 119:78-80 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wenye kiburi waaibike, maana wamenidhulumu kwa uongo, Mimi nitayatafakari mausia yako. Wakuchao na wanirudie, Nao watazijua shuhuda zako. Moyo wangu na uwe mkamilifu katika amri zako, Nisije mimi nikaaibika.
Zaburi 119:78-80 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wenye kiburi waaibike, maana wamenidhulumu kwa uongo, Mimi nitayatafakari mausia yako. Wakuchao na wanirudie, Nao watazijua shuhuda zako. Moyo wangu na uwe mkamilifu katika amri zako, Nisije mimi nikaaibika.
Zaburi 119:78-80 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Wenye majivuno na waaibishwe kwa kunikosea mimi bila sababu, lakini mimi nitatafakari juu ya mausia yako. Wale wanaokucha na wanigeukie mimi, hao ambao wanazielewa sheria zako. Moyo wangu usiwe na lawama katika kutii maagizo yako, ili nisiaibishwe.