Zaburi 111:6-9
Zaburi 111:6-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Amewaonesha watu wake nguvu ya matendo yake, amewapa nchi za mataifa mengine ziwe mali yao. Matendo yake ni ya haki na ya kuaminika; kanuni zake zote ni za kutegemewa. Amri zake zadumu daima na milele; zimetolewa kwa haki na uadilifu. Aliwakomboa watu wake na kufanya nao agano la milele. Yeye ni mtakatifu na wa kutisha mno!
Zaburi 111:6-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Amewajulisha watu wake uwezo wa matendo yake, Kwa kuwapa urithi wa mataifa. Matendo ya mikono yake ni kweli na hukumu, Maagizo yake yote ni amini, Yamethibitika milele na milele, Yamefanywa kwa uaminifu na haki. Amewapelekea watu wake ukombozi, Ameamuru agano lake liwe la milele, Jina lake ni takatifu na la kuogopwa.
Zaburi 111:6-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Amewajulisha watu wake uwezo wa matendo yake, Kwa kuwapa urithi wa mataifa. Matendo ya mikono yake ni kweli na hukumu, Maagizo yake yote ni amini, Yamethibitika milele na milele, Yamefanywa katika kweli na adili. Amewapelekea watu wake ukombozi, Ameamuru agano lake liwe la milele, Jina lake ni takatifu la kuogopwa.
Zaburi 111:6-9 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Amewaonesha watu wake uwezo wa kazi zake, akiwapa nchi za mataifa mengine. Kazi za mikono yake ni za uaminifu na haki, mausia yake yote ni ya kuaminika. Zinadumu milele na milele, zikifanyika kwa uaminifu na unyofu. Aliwapa watu wake ukombozi, aliamuru agano lake milele: jina lake ni takatifu na la kuogopwa.