Zaburi 111:1-6
Zaburi 111:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Msifuni Mwenyezi-Mungu! Nitamshukuru Mwenyezi-Mungu kwa moyo wangu wote, nikijumuika na jamii ya watu waadilifu. Matendo ya Mwenyezi-Mungu ni makuu mno! Wote wanaoyafurahia huyatafakari. Kila afanyacho kimejaa utukufu na fahari; uadilifu wake wadumu milele. Amesababisha matendo yake ya ajabu yakumbukwe; Mwenyezi-Mungu ni mwema na mwenye huruma. Huwapa chakula wenye kumcha; hasahau kamwe agano lake. Amewaonesha watu wake nguvu ya matendo yake, amewapa nchi za mataifa mengine ziwe mali yao.
Zaburi 111:1-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Haleluya. Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote, Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano. Matendo ya BWANA ni makuu, Yafikiriwa sana na wapendezwao nayo. Kazi yake imejaa heshima na adhama, Na haki yake yadumu milele. Amefanya ukumbusho wa matendo yake ya ajabu; BWANA ni mwenye fadhili na rehema. Amewapa wamchao chakula; Atalikumbuka agano lake milele. Amewajulisha watu wake uwezo wa matendo yake, Kwa kuwapa urithi wa mataifa.
Zaburi 111:1-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Haleluya. Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote, Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano. Matendo ya BWANA ni makuu, Yafikiriwa sana na wapendezwao nayo. Kazi yake ni heshima na adhama, Na haki yake yakaa milele. Amefanya ukumbusho wa matendo yake ya ajabu; BWANA ni mwenye fadhili na rehema. Amewapa wamchao chakula; Atalikumbuka agano lake milele. Amewajulisha watu wake uwezo wa matendo yake, Kwa kuwapa urithi wa mataifa.
Zaburi 111:1-6 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Msifuni BWANA. Nitamtukuza BWANA kwa moyo wangu wote, katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko. Kazi za BWANA ni kuu, wote wanaopendezwa nazo huzitafakari. Kazi zake zimejaa fahari na utukufu, haki yake hudumu daima. Amefanya maajabu yake yakumbukwe, BWANA ni mwenye neema na huruma. Huwapa chakula wale wanaomcha, hulikumbuka agano lake milele. Amewaonesha watu wake uwezo wa kazi zake, akiwapa nchi za mataifa mengine.