Methali 4:5-7
Methali 4:5-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usisahau wala kupuuza maneno yangu. Usimwache Hekima, naye atakutunza; umpende, naye atakulinda. Jambo la msingi ni kujipatia hekima; toa vyote ulivyonavyo ujipatie akili.
Methali 4:5-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau; Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu. Usimwache, naye atakusitiri; Umpende, naye atakulinda. Bora hekima, basi jipatie hekima; Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.
Methali 4:5-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Jipatie hekima, jipatie ufahamu; usiusahau; Wala usiyakatae maneno ya kinywa changu. Usimwache, naye atakuhifadhi; Umpende, naye atakulinda. Bora hekima, basi jipatie hekima; Naam, kwa mapato yako yote jipatie ufahamu.
Methali 4:5-7 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Pata hekima, pata ufahamu; usiyasahau maneno yangu wala usiyaache. Usimwache hekima naye atakuweka salama; mpende, naye atakulinda. Hekima ni bora kuliko vitu vyote; kwa hiyo jipe hekima. Hata ikikugharimu vyote ulivyo navyo, pata ufahamu.