Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 4

4
Manufaa ya hekima
1Wanangu, sikilizeni mwongozo wa baba yenu,
tegeni sikio mpate kuwa na akili.
2Maana ninawapa maagizo mema,
msiyakatae mafundisho yangu.
3Mimi pia nilikuwa mtoto mwenye baba,
nilikuwa mpole, kipenzi cha mama yangu.
4Baba yangu alinifundisha hiki:
“Zingatia kwa moyo maneno yangu,
shika amri zangu nawe utaishi.
5Jipatie hekima, jipatie ufahamu;
usisahau wala kupuuza maneno yangu.
6Usimwache Hekima, naye atakutunza;
umpende, naye atakulinda.
7Jambo la msingi ni kujipatia hekima;
toa vyote ulivyonavyo ujipatie akili.
8Mthamini sana#4:8 Mthamini sana: Maana yake katika Kiebrania si dhahiri. Hekima, naye atakutukuza;
ukimshikilia atakupa heshima.
9Atakuvika kilemba kizuri kichwani pako,
atakupa taji maridadi.”
10Mwanangu, sikia na kuyapokea maneno yangu,
ili upate kuwa na miaka mingi ya kuishi.
11Nimekufundisha njia ya hekima,
nimekuongoza katika njia nyofu.
12Ukitembea hatua zako hazitazuiwa,
wala ukikimbia hutajikwaa.
13Zingatia mafundisho ya Hekima na usimwache aponyoke,
mshike kwa makini maana yeye ni uhai wako.
14Usijiingize katika njia ya waovu,
wala usifuate mwenendo wa watu wabaya.
15Iepe njia hiyo wala usiikaribie;
jiepushe nayo, uende zako.
16Waovu kamwe hawalali wasipotenda uovu;
hawapati usingizi wasipomkwaza mtu.
17Maana uovu ndicho chakula chao,
ukatili ndiyo divai yao.
18Njia ya watu wema ni kama nuru ya alfajiri,
ambayo hungaa zaidi na zaidi hata mchana kamili.
19Lakini njia ya waovu ni kama giza nene,
hawajui kinachowafanya wajikwae.
20Mwanangu, sikiliza kwa makini maneno yangu,
itegee sikio misemo yangu.
21Usiyaache yatoweke machoni pako,
yahifadhi ndani ya moyo wako.
22Maana hayo ni uhai kwa mtu anayeyapata,
ni dawa kwa mwili wake wote.
23Linda moyo wako kwa uangalifu wote,
maana humo zatoka chemchemi za uhai.
24Tenga mbali nawe lugha potovu;
wala midomo yako isitamke maneno madanganyifu.
25Uyaelekeze macho yako mbele kwa ujasiri,
mtazamo wako uwe mbele moja kwa moja.
26 # Taz Ebr 12:13 Fikiria njia utakayochukua,
na hatua zako zote zitakuwa kamili.
27Usigeukie kulia wala kushoto;
epusha mguu wako mbali na uovu.

Iliyochaguliwa sasa

Methali 4: BHN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha