Methali 4:25-27
Methali 4:25-27 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Macho yako na yatazame mbele, kaza macho yako moja kwa moja mbele yako. Sawazisha mapito ya miguu yako na njia zako zote ziwe zimethibitika. Usigeuke kulia wala kushoto; epusha mguu wako na ubaya.
Shirikisha
Soma Methali 4Methali 4:25-27 Biblia Habari Njema (BHN)
Uyaelekeze macho yako mbele kwa ujasiri, mtazamo wako uwe mbele moja kwa moja. Fikiria njia utakayochukua, na hatua zako zote zitakuwa kamili. Usigeukie kulia wala kushoto; epusha mguu wako mbali na uovu.
Shirikisha
Soma Methali 4Methali 4:25-27 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Macho yako yatazame mbele, Na kope zako zitazame mbele yako sawasawa. Ulisawazishe pito la mguu wako, Na njia zako zote zithibitike; Usigeuke kwa kulia wala kwa kushoto; Ondoa mguu wako maovuni.
Shirikisha
Soma Methali 4