Methali 4:1-4
Methali 4:1-4 Biblia Habari Njema (BHN)
Wanangu, sikilizeni mwongozo wa baba yenu, tegeni sikio mpate kuwa na akili. Maana ninawapa maagizo mema, msiyakatae mafundisho yangu. Mimi pia nilikuwa mtoto mwenye baba, nilikuwa mpole, kipenzi cha mama yangu. Baba yangu alinifundisha hiki: “Zingatia kwa moyo maneno yangu, shika amri zangu nawe utaishi.
Methali 4:1-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wanangu, yasikilizeni mausia ya baba yenu, Tegeni masikio mpate kujua ufahamu. Kwa kuwa nawapa mafundisho mazuri; Msiiache sheria yangu. Maana nilikuwa mwana kwa baba yangu, Mpole, mpenzi wa pekee wa mama yangu. Naye akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno yangu; Shika amri zangu ukaishi.
Methali 4:1-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wanangu, yasikilizeni mausia ya baba yenu, Tegeni masikio mpate kujua ufahamu. Kwa kuwa nawapa mafundisho mazuri; Msiiache sheria yangu. Maana nalikuwa mwana kwa baba yangu, Mpole, mpenzi wa pekee wa mama yangu. Naye akanifundisha, akaniambia, Moyo wako uyahifadhi maneno yangu; Shika amri zangu ukaishi.
Methali 4:1-4 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Sikilizeni wanangu, mafundisho ya baba; sikilizeni kwa makini na mpate ufahamu. Ninawapa mafundisho ya maana, kwa hiyo msiyaache mafundisho yangu. Nilipokuwa mvulana mdogo katika nyumba ya baba yangu, ningali mchanga na mtoto pekee kwa mama yangu, baba alinifundisha akisema, “Yashike maneno yangu yote kwa moyo wako wote; yashike maagizo yangu na wewe utaishi.