Methali 26:13-16
Methali 26:13-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Mvivu husema: “Huko nje kuna simba; siwezi kwenda huko.” Kama vile mlango uzungukiapo bawaba zake, ndivyo mvivu juu ya kitanda chake. Mvivu huutia mkono wake katika sahani ya chakula, lakini hawezi kuuinua hadi mdomoni. Mvivu hujiona kuwa mwenye hekima kuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara.
Methali 26:13-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mtu mvivu husema, Simba yuko njiani, Simba yuko katika njia kuu. Kama vile mlango ugeukavyo katika bawaba zake; Kadhalika mtu mvivu katika kitanda chake. Mtu mvivu hutia mkono wake katika sahani; Kwamchosha kuupeleka tena kinywani pake. Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake, Kuliko watu saba wawezao kutoa sababu.
Methali 26:13-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mtu mvivu husema, Simba yuko njiani, Simba yuko katika njia kuu. Kama vile mlango ugeukavyo katika bawaba zake; Kadhalika mtu mvivu katika kitanda chake. Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini; Kwamchosha kuupeleka tena kinywani pake. Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake, Kuliko watu saba wawezao kutoa sababu.
Methali 26:13-16 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Mvivu husema, “Yuko simba barabarani, simba mkali anazunguka mitaa!” Kama vile mlango ugeukavyo kwenye bawaba zake, ndivyo mvivu ajigeuzavyo kitandani mwake. Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani, naye huchoka kuupeleka kwenye kinywa chake. Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake mwenyewe, kuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara.