Methali 23:6-8
Methali 23:6-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Usile chakula cha mtu bahili, wala usitamani mapochopocho yake, maana moyoni mwake anahesabu unachokula. Atakuambia, “Kula, kunywa!” Lakini moyoni mwake hayuko pamoja nawe. Utatapika vipande ulivyokula; shukrani zako zote zitakuwa za bure.
Methali 23:6-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Usile mkate wa mtu mwenye husuda; Wala usivitamani vyakula vyake vya anasa; Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe. Tonge lile ulilokula utalitapika, Na maneno yako matamu yatakupotea.
Methali 23:6-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Usile mkate wa mtu mwenye husuda; Wala usivitamani vyakula vyake vya anasa; Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe. Tonge lile ulilokula utalitapika, Na maneno yako matamu yatakupotea.
Methali 23:6-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Usile chakula cha mtu mchoyo, usitamani vyakula vyake vitamu, kwa maana yeye ni aina ya mtu ambaye kila mara anafikiri kuhusu gharama. Anakuambia, “Kula na kunywa,” lakini moyo wake hauko pamoja nawe. Utatapika kile kidogo ulichokula, nawe utakuwa umepoteza bure maneno yako ya kumsifu.