Mithali 23:6-8
Mithali 23:6-8 NENO
Usile chakula cha mtu mchoyo, usitamani vyakula vyake vitamu, kwa maana yeye ni aina ya mtu ambaye kila mara anafikiri kuhusu gharama. Anakuambia, “Kula na kunywa,” lakini moyo wake hauko pamoja nawe. Utatapika kile kidogo ulichokula, nawe utakuwa umepoteza bure maneno yako ya kumsifu.