Methali 13:10-19
Methali 13:10-19 Biblia Habari Njema (BHN)
Kiburi husababisha tu ugomvi, lakini kwa wanaokubali shauri jema mna hekima. Mali ya harakaharaka hutoweka, lakini akusanyaye kidogokidogo ataiongeza. Tumaini la kungojangoja huumiza moyo, lakini tazamio linalotimia ni mti wa uhai. Anayedharau mawaidha anajiletea maangamizi, lakini anayetii amri atapewa tuzo. Mafundisho ya wenye hekima ni chemchemi ya uhai; humwezesha mtu kuiepa mitego ya kifo. Kuwa na akili huleta fadhili, lakini njia ya waovu ni ya taabu Mwenye busara hutenda kila kitu kwa akili, lakini mpumbavu hutembeza upumbavu wake. Mjumbe mbaya huwatumbukiza watu taabuni, lakini mjumbe mwaminifu huleta nafuu. Umaskini na fedheha humpata asiyejali mafundisho, lakini mwenye kusikia maonyo huheshimiwa. Inafurahisha upatapo kile unachotaka, kwa hiyo wapumbavu huchukia kuepa uovu.
Methali 13:10-19 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana. Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa. Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima. Kila anayelidharau neno hujiletea uharibifu; Bali yeye anayeiogopa amri atapewa thawabu. Sheria ya mwenye akili ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti. Ufahamu mwema huleta upendeleo; Bali njia ya muasi huangamiza. Kila aliye na busara hutenda kazi kwa maarifa; Bali mpumbavu hueneza upumbavu. Mjumbe mbaya huanguka maovuni; Bali mjumbe mwaminifu ni afya. Umaskini na fedheha zitampata yeye akataaye kurudiwa; Bali yeye aangaliaye maonyo ataheshimiwa. Haja iliyopatikana ni tamu nafsini mwa mtu; Bali kujitenga na maovu ni chukizo kwa wapumbavu.
Methali 13:10-19 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana. Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa. Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima. Kila alidharauye neno hujiletea uharibifu; Bali yeye aiogopaye amri atapewa thawabu. Sheria ya mwenye akili ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti. Ufahamu mwema huleta upendeleo; Bali njia ya haini huparuza. Kila aliye na busara hutenda kazi kwa maarifa; Bali mpumbavu hueneza upumbavu. Mjumbe mbaya huanguka maovuni; Bali mjumbe mwaminifu ni afya. Umaskini na fedheha zitampata yeye akataaye kurudiwa; Bali yeye aangaliaye maonyo ataheshimiwa. Haja iliyopatikana ni tamu nafsini mwa mtu; Bali kujitenga na maovu ni chukizo kwa wapumbavu.
Methali 13:10-19 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Kiburi huzalisha magomvi tu, bali hekima hupatikana kwa wale wanaozingatia ushauri. Fedha isiyo ya halali hupungua, bali yeye akusanyaye fedha kidogo kidogo huongezeka. Kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua, bali tumaini lililotimizwa ni mti wa uzima. Yeye anayedharau mafundisho anajiletea maangamizi, bali yeye anayeheshimu agizo hupewa tuzo. Mafundisho ya mwenye busara ni chemchemi ya uzima, ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti. Ufahamu mzuri hupata upendeleo, bali njia ya asiye mwaminifu ni ngumu. Kila mwenye busara hutenda kwa maarifa, bali mpumbavu hudhihirisha upumbavu wake. Mjumbe mwovu huanguka kwenye taabu, bali mjumbe mwaminifu huleta uponyaji. Yeye anayedharau maonyo hupata umaskini na aibu, bali yeye anayekubali maonyo huheshimiwa. Tarajio lililotimizwa ni tamu kwa nafsi, bali wapumbavu huchukia sana kuacha ubaya.