Mit 13:10-19
Mit 13:10-19 SUV
Kiburi huleta mashindano tu; Bali hekima hukaa nao wanaoshauriana. Mali iliyopatikana kwa haraka itapunguka; Bali yeye achumaye kidogo kidogo atazidishiwa. Kilichotarajiwa kikikawia kuja, moyo huugua. Bali haja ya mtu ikipatikana, ni mti wa uzima. Kila alidharauye neno hujiletea uharibifu; Bali yeye aiogopaye amri atapewa thawabu. Sheria ya mwenye akili ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti. Ufahamu mwema huleta upendeleo; Bali njia ya haini huparuza. Kila aliye na busara hutenda kazi kwa maarifa; Bali mpumbavu hueneza upumbavu. Mjumbe mbaya huanguka maovuni; Bali mjumbe mwaminifu ni afya. Umaskini na fedheha zitampata yeye akataaye kurudiwa; Bali yeye aangaliaye maonyo ataheshimiwa. Haja iliyopatikana ni tamu nafsini mwa mtu; Bali kujitenga na maovu ni chukizo kwa wapumbavu.