Mathayo 1:22-25
Mathayo 1:22-25 Biblia Habari Njema (BHN)
Basi, haya yote yalitukia ili litimie lile neno Bwana alilosema kwa njia ya nabii: “Bikira atachukua mimba, atamzaa mtoto wa kiume, nao watampa jina Emanueli” (maana yake, “Mungu yuko nasi”). Hivyo, Yosefu alipoamka usingizini alifanya kama malaika huyo alivyomwambia, akamchukua mke wake nyumbani. Lakini hakulala naye hata Maria alipojifungua mtoto wa kiume. Naye Yosefu akampa jina Yesu.
Mathayo 1:22-25 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema, Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi. Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe; asimjue kamwe hadi alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU.
Mathayo 1:22-25 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema, Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi. Naye Yusufu alipoamka katika usingizi, alifanya kama malaika wa Bwana alivyomwagiza; akamchukua mkewe; asimjue kamwe hata alipomzaa mwanawe; akamwita jina lake YESU.
Mathayo 1:22-25 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Haya yote yalitukia ili litimie lile Bwana alilonena kupitia nabii, aliposema: “Tazama, bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, nao watamwita jina Imanueli” (maana yake, “Mungu pamoja nasi”). Yusufu alipoamka kutoka usingizini, akafanya jinsi alivyoagizwa na malaika wa Bwana, akamchukua Mariamu kuwa mke wake. Lakini hawakukutana kimwili hadi Mariamu alipojifungua mwanawe; akamwita jina Yesu.