Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia 51:60-62 - Compare All Versions

Yeremia 51:60-62 BHN (Biblia Habari Njema)

Nilikuwa nimeandika kitabuni maafa yote niliyotangaza juu ya Babuloni na pia maneno mengine kuhusu Babuloni. Nilimwambia Seraya: “Utakapofika Babuloni ni lazima uwasomee wote ujumbe huu. Kisha umalizie na maneno haya: ‘Ee Mwenyezi-Mungu, wewe umesema kwamba utapaharibu mahali hapa hata pasikaliwe na kiumbe chochote, mwanadamu au mnyama, na kwamba nchi hii itakuwa jangwa milele.’

Shirikisha
Yeremia 51 BHN

Yeremia 51:60-62 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Naye Yeremia akaandika katika kitabu kuhusu mabaya yote yatakayoupata Babeli, maneno hayo yote yaliyoandikwa juu ya Babeli. Naye Yeremia akamwambia Seraya, Utakapofika Babeli, basi angalia uyasome maneno haya yote, ukaseme, Ee BWANA, umenena kuhusu mji huu kwamba utakatiliwa mbali, usikaliwe na awaye yote, wala wanadamu wala wanyama, lakini uwe ukiwa hata milele.

Shirikisha
Yeremia 51 SRUV

Yeremia 51:60-62 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Naye Yeremia akaandika katika kitabu habari ya mabaya yote yatakayoupata Babeli, maneno hayo yote yaliyoandikwa juu ya Babeli. Naye Yeremia akamwambia Seraya, Utakapofika Babeli, basi angalia uyasome maneno haya yote, ukaseme, Ee BWANA, umenena habari za mji huu kwamba utakatiliwa mbali, usikaliwe na awaye yote, wala wanadamu wala wanyama, lakini uwe ukiwa hata milele.

Shirikisha
Yeremia 51 SUV

Yeremia 51:60-62 NEN (Neno)

Yeremia alikuwa ameandika ndani ya kitabu kuhusu maafa yote yatakayoipata Babeli, yaani yote yaliyokuwa yameandikwa kuhusu Babeli. Yeremia akamwambia Seraya, “Utakapofika Babeli, hakikisha kwamba umesoma maneno haya yote kwa sauti kubwa. Kisha sema, ‘Ee BWANA, umesema utaangamiza mahali hapa ili mtu wala mnyama asiishi ndani yake, napo patakuwa ukiwa milele.’

Shirikisha
Yeremia 51 NEN