Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia 51

51
1 # 2 Fal 19:7; Yer 4:11 BWANA asema hivi, Angalia, nitaamsha juu ya Babeli, na juu yao wakaao Leb-kamai,#51:1 Leb-kamai: yaani Ukaldayo, kwa fumbo. upepo uharibuo. 2#Yer 15:7; 50:14 Nami nitawatuma wapepetaji watakaompepea mpaka Babeli, nao wataifanya nchi yake kuwa tupu; kwa kuwa katika siku ya taabu watakuwa juu yake pande zote. 3Juu yake apindaye upinde, mwenye upinde na apinde upinde wake, na juu yake ajiinuaye katika dirii yake; msiwaachilie vijana wake; liangamizeni jeshi lake lote. 4#Yer 49:26 Nao wataanguka, wakiwa wameuawa, katika nchi ya Wakaldayo, wakiwa wametumbuliwa katika njia zake kuu. 5#Zab 91:14; Zek 1:15 Kwa maana Israeli, wala Yuda, hakuachwa na Mungu wake, BWANA wa majeshi; ijapokuwa nchi yao imejaa hatia juu yake aliye Mtakatifu wa Israeli. 6#Ufu 18:4; Yer 25:14 Kimbieni kutoka kati ya Babeli, kila mtu na ajiokoe nafsi yake; msikatiliwe mbali katika uovu wake; maana ni wakati wa kisasi cha BWANA, atamlipa malipo. 7#Ufu 17:2-4; 18:3; Yer 25:16 Babeli umekuwa kikombe cha dhahabu mkononi mwa BWANA; kilicholevya dunia yote; mataifa wamekunywa mvinyo wake; kwa sababu hiyo mataifa wameingiwa na wazimu. 8#Isa 21:9; 1 The 5:12; Ufu 18:9; Yer 46:11 Babeli umeanguka na kuangamia ghafla; mwombolezeni; twaeni zeri kwa maumivu yake; ili labda apate kuponywa.
9 # Ufu 18:5; Isa 13:14; Yer 46:16 Tungependa kuuponya Babeli,
Lakini haukuponyeka;
Mwacheni, nasi twendeni zetu,
Kila mtu hata nchi yake mwenyewe;
Maana hukumu yake inafika hata mbinguni,
Nayo imeinuliwa kufikia mawinguni.
10 # Zab 37:6 BWANA ameitokeza haki yetu;
Njooni, tutangaze katika Sayuni
Habari za kazi ya BWANA, Mungu wetu.
11 # Isa 13:17 Inoeni hiyo mishale; zishikeni ngao kwa nguvu; BWANA ameziamsha roho za wafalme wa Wamedi; kwa sababu shauri lake ni juu ya Babeli auangamize; maana ni kisasi cha BWANA, kisasi cha hekalu lake. 12#Nah 2:1 Twekeni bendera ya vita juu ya kuta za Babeli, imarisheni ulinzi, wawekeni walinzi, tayarisheni waviziao; kwa maana BWANA ameazimia na kutenda yote aliyoyasema juu yao wakaao Babeli. 13#Ufu 17:1 Ewe ukaaye juu ya maji mengi, uliye na hazina nyingi, mwisho wako umewadia, kadiri ya tamaa zako. 14#Yer 49:13; Nah 3:15 BWANA wa majeshi ameapa kwa nafsi yake, akisema, Hakika nitakujaza watu, kama nzige, nao watapiga kelele juu yako.
15 # Mwa 1:1; Zab 146:5,6; Isa 49:26; Mdo 14:15; Kol 1:16,17; Ebr 1:2,3; Ayu 9:8 Ameiumba dunia kwa uweza wake,
Ameuthibitisha ulimwengu kwa hekima yake,
Na kwa ufahamu wake amezitandika mbingu.
16 # Zab 135:7 Atoapo sauti yake pana kishindo cha maji mbinguni,
Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi;
Huifanyia mvua umeme,
Huutoa upepo katika hazina zake.
17 # Yer 50:2 Kila mtu amekuwa kama mnyama, hana maarifa;
Kila mfua dhahabu amefedheheshwa na sanamu yake ya kuchonga;
Maana sanamu yake ya kuyeyuka ni uongo,
Wala hamna pumzi ndani yake.
18 # Yon 2:8 Ni ubatili tu, ni kazi za udanganyifu;
Wakati wa kujiliwa kwao watapotea.
19 # Zab 16:5; 73:26; Yer 10:16; Omb 3:24 Yeye, Fungu la Yakobo, siye kama hawa;
Maana ndiye aliyeviumba vitu vyote;
Na Israeli ni kabila la urithi wake;
BWANA wa majeshi ndilo jina lake.
Israeli aliye chombo cha muumbaji
20 # Isa 10:5; Yer 50:23 Wewe ni rungu langu na silaha zangu za vita; kwa wewe nitawavunjavunja mataifa; na kwa wewe nitaharibu falme; 21na kwa wewe nitamvunjavunja farasi, na yeye ampandaye; na kwa wewe nitalivunjavunja gari la vita, na yeye achukuliwaye ndani yake; 22#2 Nya 36:17 na kwa wewe nitawavunjavunja mwanamume na mwanamke; na kwa wewe nitawavunjavunja mzee na mtoto; na kwa wewe nitawavunjavunja kijana mwanamume na kijana mwanamke; 23na kwa wewe nitamvunjavunja mchungaji na kundi lake; na kwa wewe nitamvunjavunja mkulima na jozi yake ya ng'ombe; na kwa wewe nitawavunjavunja watawala na makamanda.
Maangamizi ya Babeli
24 # Yer 50:15,16 Nami nitamlipa Babeli, na wote wakaao ndani ya Ukaldayo, mabaya yao yote, waliyoyatenda katika Sayuni mbele ya macho yenu, asema BWANA.
25 # Isa 13:2; Zek 4:7; Ufu 8:8 Tazama, mimi niko juu yako, Ee mlima uharibuo, asema BWANA; wewe uiharibuye dunia nzima; nami nitaunyosha mkono wangu juu yako, na kukubingirisha chini toka majabalini; nami nitakufanya kuwa mlima ulioteketezwa. 26Wala hawatatwaa kwako jiwe moja liwe la pembeni, wala jiwe moja liwe msingi; bali wewe utakuwa ukiwa daima, asema BWANA. 27#Isa 13:2; Yer 15:14; 50:41 Itwekeni bendera katika nchi, pigeni tarumbeta kati ya mataifa, yawekeni mataifa tayari juu yake; ziiteni juu yake falme za Ararati, na Mini, na Ashkenazi; agizeni jemadari juu yake; wapandisheni farasi, kama tunutu. 28Wekeni mataifa tayari juu yake, wafalme wa Wamedi, na watawala wake, na wakuu wake, na nchi yote ya mamlaka yake. 29#Yer 50:13 Nayo nchi yatetemeka, nayo ina uchungu; maana makusudi ya BWANA juu ya Babeli yasimama, kuifanya nchi ya Babeli ukiwa, isikaliwe na mtu.
30 # Isa 19:16; Omb 1:9; Amo 1:5 Mashujaa wa Babeli wameacha kupigana;
Wanakaa katika ngome zao;
Ushujaa wao umewapungukia;
Wamekuwa kama wanawake;
Makao yake yameteketea;
Makomeo yake yamevunjika.
31 # Yer 50:24 Tarishi mmoja atapiga mbio kumlaki mwingine,
Na mjumbe mmoja atapiga mbio kumlaki mwenziwe,
Ili kumpasha habari mfalme wa Babeli,
Ya kuwa mji wake umetwaliwa kila upande.
32Navyo vivuko vimeshambuliwa,
Nayo makangaga wameyatia moto,
Nao watu wa vita wameingiwa na hofu.
33 # Isa 21:10; Yoe 3:13; Mt 13:30 Kwa maana BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi; Binti Babeli amekuwa kama sakafu ya kufikichia wakati wa kukanyagwa kwake; bado kitambo kidogo na wakati wa mavuno utafika kwake. 34#2 Nya 36:9,10; Yer 24:1 Nebukadneza, mfalme wa Babeli, amenila, ameniponda, amenifanya kuwa chombo kitupu; amenimeza kama joka, amelijaza tumbo lake vitu vyangu vya anasa; amenitupa 35Udhalimu niliotendwa mimi, na uliotendwa mwili wangu, umpate Babeli; ndivyo atakavyosema yeye akaaye Sayuni; na Yerusalemu atasema, Damu yangu na iwe juu yao wakaao katika Ukaldayo. 36#Zek 1:15; Yer 50:38 Basi, BWANA asema hivi, Tazama, nitakutetea, nami nitatwaa kisasi kwa ajili yako; nami nitaikausha bahari yake, nitaifanya chemchemi yake kuwa pakavu. 37#Isa 13:22; 2 Nya 29:8; Yer 18:16 Na Babeli utakuwa magofu, makao ya mbwamwitu, ajabu, na mazomeo, pasipo mtu wa kukaa huko. 38Watanguruma pamoja kama wanasimba; watanguruma kama simba wachanga. 39#Dan 5:1,30 Wakiingiwa na ukali, nitawafanyia karamu yao, nami nitawalevya, wapate kufurahi, na kulala usingizi wa milele, wasiamke tena, asema BWANA. 40Nitawateremsha kama wana-kondoo machinjoni, kama kondoo dume pamoja na mabeberu.
41 # Yer 25:26; 49:25; Isa 13:19; Dan 4:30 Jinsi Sheshaki#51:41 Sheshaki: yaani Babeli, kwa fumbo. alivyotwaliwa!
Naye sifa ya dunia yote alivyoshambuliwa!
Jinsi Babeli alivyokuwa ukiwa
Katikati ya mataifa!
42 # Isa 8:7,8 Bahari imefika juu ya Babeli,
Umefunikwa kwa wingi wa mawimbi yake.
43Miji yake imekuwa maganjo;
Nchi ya ukame, na jangwa;
Nchi asimokaa mtu yeyote,
Wala hapiti mwanadamu huko.
44 # Yer 50:2 Nami nitafanya hukumu juu ya Beli katika Babeli, nami nitavitoa katika kinywa chake alivyovimeza; wala mataifa hawatamwendea tena; naam, ukuta wa Babeli utaanguka.
45 # Ufu 18:4 Enyi watu wangu; tokeni katikati yake, mkajiokoe nafsi zenu kutoka kwa hasira kali ya BWANA, kila mmoja wenu. 46#2 Fal 19:7 Wala isizimie mioyo yenu, wala msiiogope habari itakayosikiwa katika nchi; maana habari itakuja mwaka mmoja, na baadaye mwaka wa pili habari itakuja, na udhalimu katika nchi, mwenye kutawala akishindana na mwenye kutawala. 47#Isa 44:23; Yer 50:3 Basi angalia, siku zitakuja, ambazo katika siku hizo, nitafanya hukumu juu ya sanamu za Babeli, na nchi yake yote itatahayarika; na watu wake wote waliouawa wataanguka katikati yake. 48#Ufu 18:20; Yer 44:28 Ndipo mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo, vitaimba kwa furaha juu ya Babeli; kwa maana watu waangamizao watamjia kutoka kaskazini, asema BWANA. 49#Ufu 18:24 Kama vile Babeli alivyowaangusha watu wa Israeli waliouawa, ndivyo watakavyoanguka katika Babeli watu wa nchi yake nzima waliouawa.
50 # Yer 44:28 Ninyi mliojiepusha na upanga,
Nendeni zenu, msisimame;
Mkumbukeni BWANA tokea mbali,
Na Yerusalemu ukatiwe mioyoni mwenu.
51 # Zab 44:15 Twaona haya kwa kuwa tumesikia shutuma;
Fedheha imetufunika nyuso zetu;
Kwa sababu wageni wamepaingia
Patakatifu pa nyumba ya BWANA.
52Kwa sababu hiyo siku zinakuja, asema BWANA, nitakapozihukumu sanamu zake; na katika nchi yake yote waliojeruhiwa wataomboleza. 53#Yer 49:16; Amo 9:2 Babeli ujapopanda mbinguni, na ujapopafanya mahali pa juu penye nguvu zake kuwa ngome, hata hivyo toka kwangu wenye kuangamiza watamwendea, asema BWANA.
54 # Isa 13:6-9; 15:5; Yer 50:22; Sef 1:10 Sauti ya kilio kutoka Babeli,
Na ya uangamizi mkuu toka nchi ya Wakaldayo!
55Maana BWANA amwangamiza Babeli,
Na kuikomesha sauti kuu ndani yake;
Na mawimbi yake yavuma kama maji mengi,
Mshindo wa sauti zao wafanya makelele;
56 # Kum 32:35; Zab 94:1 Kwa maana mwenye kuangamiza amefika kwake;
Naam, amefika Babeli;
Na mashujaa wake wametwaliwa;
Pinde zao zimevunjika kabisa;
Maana BWANA ni Mungu wa kisasi;
Hakika yake yeye atalipa.
57 # Yer 46:18; 48:15 Nami nitawalevya wakuu wake, na watu wake wenye hekima, watawala wake, na makamanda wake, na mashujaa wake; nao watalala usingizi wa milele, wasiamke, asema Mfalme, BWANA wa majeshi, ambaye jina lake ni BWANA. 58#Hab 2:13 BWANA wa majeshi asema hivi, Kuta pana za Babeli zitabomolewa kabisa, na malango yake marefu yatateketezwa; nao watu watajitaabisha kwa ubatili, na mataifa kwa moto; nao watachoka.
Yeremia amwamuru Seraya
59Neno ambalo Yeremia, nabii, alimwamuru Seraya, mwana wa Neria, mwana wa Maaseya, alipokwenda Babeli pamoja na Sedekia, mfalme wa Yuda, katika mwaka wa nne wa kumiliki kwake. Basi Seraya alikuwa msimamizi mkuu wa nyumba ya mfalme. 60Naye Yeremia akaandika katika kitabu kuhusu mabaya yote yatakayoupata Babeli, maneno hayo yote yaliyoandikwa juu ya Babeli. 61Naye Yeremia akamwambia Seraya, Utakapofika Babeli, basi angalia uyasome maneno haya yote, 62#Yer 50:3,39 ukaseme, Ee BWANA, umenena kuhusu mji huu kwamba utakatiliwa mbali, usikaliwe na awaye yote, wala wanadamu wala wanyama, lakini uwe ukiwa hata milele. 63#Ufu 18:21 Tena itakuwa utakapokwisha kukisoma kitabu hicho, utakifungia jiwe, na kukitupa katika mto Frati; 64nawe utasema, Hivyo ndivyo utakavyozama Babeli, wala hautazuka tena, kwa sababu ya mabaya yote nitakayoleta juu yake; nao watachoka.
Maneno ya Yeremia yamefika hata hapa.

Iliyochaguliwa sasa

Yeremia 51: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia