Yeremia 51:48-50
Yeremia 51:48-50 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha mbingu, dunia na vyote vilivyomo vitaimba kwa furaha kuhusu kuanguka kwa Babuloni, waangamizi watakapofika kutoka kaskazini kuushambulia. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.” Babuloni umesababisha vifo duniani kote; sasa wenyewe utaangamizwa kwa mauaji ya Israeli. “Nyinyi mlinusurika kifo, ondokeni sasa, wala msisitesite! Ingawa mko nchi ya mbali mkumbukeni Mwenyezi-Mungu, ukumbukeni pia mji wa Yerusalemu.
Yeremia 51:48-50 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo, vitaimba kwa furaha juu ya Babeli; kwa maana watu waangamizao watamjia kutoka kaskazini, asema BWANA. Kama vile Babeli alivyowaangusha watu wa Israeli waliouawa, ndivyo watakavyoanguka katika Babeli watu wa nchi yake nzima waliouawa. Ninyi mliojiepusha na upanga, Nendeni zenu, msisimame; Mkumbukeni BWANA tokea mbali, Na Yerusalemu ukatiwe mioyoni mwenu.
Yeremia 51:48-50 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo mbingu, na nchi, na vitu vyote vilivyomo, vitaimba kwa furaha juu ya Babeli; kwa maana watu waangamizao watamjilia kutoka kaskazini, asema BWANA. Kama vile Babeli alivyowaangusha watu wa Israeli waliouawa, ndivyo watakavyoanguka katika Babeli watu wa nchi yake nzima waliouawa. Ninyi mliojiepusha na upanga, Enendeni zenu, msisimame; Mkumbukeni BWANA tokea mbali, Na Yerusalemu ukatiwe mioyoni mwenu.
Yeremia 51:48-50 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ndipo mbingu na dunia na vyote vilivyomo ndani yake vitapiga kelele za shangwe juu ya Babeli, kwa kuwa kutoka kaskazini waharabu watamshambulia,” asema BWANA. “Babeli ni lazima aanguke kwa sababu ya kuwaua Waisraeli, kama vile waliouawa duniani kote walivyoanguka kwa sababu ya Babeli. Wewe uliyepona upanga, ondoka wala usikawie! Mkumbuke BWANA ukiwa katika nchi ya mbali, na utafakari juu ya Yerusalemu.”