Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia 5:1-2 - Compare All Versions

Yeremia 5:1-2 BHN (Biblia Habari Njema)

Kimbieni huko na huko mjini Yerusalemu; pelelezeni na kujionea wenyewe! Chunguzeni masoko yake mwone kama kuna mtu atendaye haki mtu atafutaye ukweli; akiwako, basi Mwenyezi-Mungu atausamehe Yerusalemu. Ingawa wanaapa: “Kama Mwenyezi-Mungu aishivyo”, viapo vyao ni vya uongo.

Shirikisha
Yeremia 5 BHN

Yeremia 5:1-2 SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)

Pigeni mbio huku na huku katika njia za Yerusalemu, mkaone sasa, na kujua, na kutafuta katika viwanja vyake, kwamba mwaweza kumpata mtu mmoja, kwamba yuko mtu mmoja awaye yote atendaye kwa haki, atafutaye uaminifu; nami nitausamehe mji huo. Na wajaposema, Kama BWANA aishivyo, hakika waapa kwa uongo.

Shirikisha
Yeremia 5 SUV

Yeremia 5:1-2 SRUV (Swahili Revised Union Version)

Pigeni mbio huku na huku katika njia za Yerusalemu, mkaone sasa, na kujua, na kutafuta katika viwanja vyake, kwamba mwaweza kumpata mtu mmoja, kwamba yuko mtu mmoja awaye yote atendaye kwa haki, atafutaye uaminifu; nami nitausamehe mji huo. Na wajaposema, Kama BWANA aishivyo, hakika waapa kwa uongo.

Shirikisha
Yeremia 5 SRUV

Yeremia 5:1-2 NEN (Neno)

“Pandeni na kushuka katika mitaa ya Yerusalemu, tazameni pande zote na mtafakari, tafuteni katika viwanja vyake. Kama mtaweza kumpata hata mtu mmoja tu atendaye kwa uaminifu na kutafuta kweli, nitausamehe mji huu. Ingawa wanasema, ‘Kwa hakika kama BWANA aishivyo,’ bado wanaapa kwa uongo.”

Shirikisha
Yeremia 5 NEN