Isaya 54:2-3
Isaya 54:2-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Panua nafasi hemani mwako, tandaza mapazia hapo unapoishi, usijali gharama zake. Zirefushe kamba zake, na kuimarisha vigingi vyake; maana utapanuka kila upande; wazawa wako watamiliki mataifa, miji iliyokuwa mahame itajaa watu.
Isaya 54:2-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako. Kwa maana utaenea upande wa kulia na upande wa kushoto; na wazao wako watawamiliki mataifa; wataifanya miji iliyokuwa ukiwa kukaliwa na watu.
Isaya 54:2-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Panua mahali pa hema yako, na wayatandaze mapazia ya maskani yako; usiwakataze; ongeza urefu wa kamba zako; vikaze vigingi vya hema yako. Kwa maana utaenea upande wa kuume na upande wa kushoto; na wazao wako watawamiliki mataifa; wataifanya miji iliyokuwa ukiwa kukaliwa na watu.
Isaya 54:2-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Panua mahali pa hema lako, tandaza mapazia ya hema lako uyaeneze mbali, wala usiyazuie; ongeza urefu wa kamba zako, imarisha vigingi vyako. Kwa maana utaenea upande wa kuume na upande wa kushoto; wazao wako watayamiliki mataifa na kukaa katika miji yao iliyoachwa ukiwa.