Waebrania 4:7-8
Waebrania 4:7-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu aliweka siku nyingine ambayo inaitwa “Leo,” akasema baadaye kwa njia ya Daudi maneno yaliyokwisha tajwa: “Kama mkisikia sauti ya Mungu leo, msiwe wakaidi.” Kama Yoshua angekuwa amewapa watu hao hilo pumziko, Mungu hangalisema baadaye juu ya siku nyingine.
Waebrania 4:7-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
aweka tena siku fulani, akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii, Leo, kama ilivyonenwa tangu zamani, Leo, kama mkisikia sauti yake, Msifanye mioyo yenu migumu. Maana kama Yoshua angaliwapa pumziko, asingaliinena siku nyingine baadaye.
Waebrania 4:7-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
aweka tena siku fulani, akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii, Leo; kama ilivyonenwa tangu zamani, Leo, kama mtaisikia sauti yake, Msifanye migumu mioyo yenu. Maana kama Yoshua angaliwapa raha, asingaliinena siku nyingine baadaye.
Waebrania 4:7-8 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kwa hiyo Mungu ameweka siku nyingine, akaiita Leo, akisema kwa kinywa cha Daudi baadaye sana, kwa maneno yaliyotangulia kunenwa: “Leo, kama mkiisikia sauti yake, msiifanye mioyo yenu migumu.” Kwa maana kama Yoshua alikuwa amewapa raha, Mungu hangesema tena baadaye kuhusu siku nyingine.