Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waraka kwa Waebrania 4

4
Pumziko aliloahidi Mungu
1 # Zab 95:11 Basi, ikiwa ingalipo ahadi ya kuingia katika pumziko lake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa. 2Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa Habari Njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia. 3#Zab 95:11 Maana sisi tulioamini tunaingia katika pumziko lile; kama vile alivyosema,
Kama nilivyoapa kwa hasira yangu,
Hawataingia pumzikoni mwangu:
ijapokuwa zile kazi zilimalizika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu. 4#Mwa 2:2 Kwa maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote; 5#Zab 95:11 na tena kunena hapa napo, Hawataingia pumzikoni mwangu. 6Basi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia humo, na wale waliohubiriwa habari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao, 7#Zab 95:7-8 aweka tena siku fulani, akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii, Leo, kama ilivyonenwa tangu zamani,
Leo, kama mkisikia sauti yake,
Msifanye mioyo yenu migumu.
8 # Kum 31:7; Yos 22:4 Maana kama Yoshua angaliwapa pumziko, asingaliinena siku nyingine baadaye. 9Basi, limesalia pumziko la sabato kwa watu wa Mungu. 10#Mwa 2:2; Ufu 14:13 Kwa maana yeye aliyeingia katika pumziko lake amepumzika mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyopumzika katika kazi zake. 11Basi, na tufanye bidii kuingia katika pumziko lile, ili kwamba mtu yeyote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi. 12#Yer 23:29; Isa 49:2; Efe 6:17; Yn 12:48; Ufu 19:15 Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena ni jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. 13Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, maana vitu vyote ni tupu na kuwekwa wazi machoni pake yeye ambaye tunapaswa kuwajibika kwake.
Yesu aliye Kuhani Mkuu
14 # Ebr 3:1; 6:20; 7:26; 8:1; 9:11 Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. 15#Ebr 2:17 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa kama sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. 16#1 Yoh 3:21; Rum 3:25 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.

Iliyochaguliwa sasa

Waraka kwa Waebrania 4: SRUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha