Mwanzo 24:52-53
Mwanzo 24:52-53 Biblia Habari Njema (BHN)
Mtumishi wa Abrahamu aliposikia maneno hayo, alimsujudia Mwenyezi-Mungu. Kisha akatoa vito vya fedha na dhahabu na nguo, akampa Rebeka. Pia aliwapa ndugu na mama yake Rebeka mapambo ya thamani kubwa.
Mwanzo 24:52-53 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ikawa mtumishi wa Abrahamu aliposikia maneno yao, akainama hata nchi mbele za BWANA. Kisha huyo mtumishi akatoa vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi, akampa Rebeka; na vitu vya thamani akampa nduguye na mamaye pia.
Mwanzo 24:52-53 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ikawa mtumishi wa Ibrahimu aliposikia maneno yao, akainama hata nchi mbele za BWANA. Kisha huyo mtumishi akatoa vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi, akampa Rebeka; na vitu vya thamani akampa nduguye na mamaye pia.
Mwanzo 24:52-53 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Ikawa huyo mtumishi wa Abrahamu aliposikia waliyosema, alisujudu, uso wake ukagusa chini mbele za BWANA. Ndipo huyo mtumishi akatoa vitu vilivyotengenezwa kwa dhahabu na kwa fedha, pamoja na mavazi, akampa Rebeka; pia akawapa zawadi za thamani kubwa nduguye na mamaye.