Mwanzo 24:52-53
Mwanzo 24:52-53 SRUV
Ikawa mtumishi wa Abrahamu aliposikia maneno yao, akainama hata nchi mbele za BWANA. Kisha huyo mtumishi akatoa vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na mavazi, akampa Rebeka; na vitu vya thamani akampa nduguye na mamaye pia.


