Kumbukumbu la Sheria 33:1-2
Kumbukumbu la Sheria 33:1-2 Biblia Habari Njema (BHN)
Hii ndiyo baraka ambayo Mose, mtu wa Mungu aliwatakia Waisraeli kabla ya kufariki kwake. Alisema: Mwenyezi-Mungu alikuja kutoka mlima Sinai, alitutokea kutoka mlima Seiri; aliiangaza kutoka mlima Parani. Alitokea kati ya maelfu ya malaika, na moto uwakao katika mkono wake wa kulia.
Kumbukumbu la Sheria 33:1-2 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hii ndiyo baraka ya Musa, huyo mtu wa Mungu, aliyowabarikia wana wa Israeli kabla ya kufa kwake. Akasema, BWANA alitoka Sinai, Akawajia kutoka Seiri; Aliangaza katika kilima cha Parani, Akaja Meribath-kadeshi. Upande wa mkono wake wa kulia Palikuwa na sheria ya motomoto kwao.
Kumbukumbu la Sheria 33:1-2 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hii ndiyo baraka ya Musa, huyo mtu wa Mungu, aliyowabarikia wana wa Israeli kabla ya kufa kwake. Akasema, BWANA alitoka Sinai, Akawaondokea kutoka Seiri; Aliangaza katika kilima cha Parani, Akaja Meribath-kadeshi. Upande wa mkono wake wa kuume Palikuwa na sheria ya moto-moto kwao.
Kumbukumbu la Sheria 33:1-2 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hii ndiyo baraka Mose mtu wa Mungu aliyotamka kwa Waisraeli kabla ya kifo chake. Alisema: “BWANA alikuja kutoka Mlima Sinai, akachomoza kama jua juu yao kutoka Mlima Seiri, akaangaza kutoka Mlima Parani. Alikuja pamoja na watakatifu makumi elfu kutoka kusini, kutoka materemko ya mlima wake.