1 Samueli 15:1-3
1 Samueli 15:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Samueli alimwambia Shauli, “Mwenyezi-Mungu alinituma kukupaka mafuta uwe mfalme wa watu wake wa Israeli. Sasa sikiliza maneno ya Mwenyezi-Mungu. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: ‘Nitawaadhibu Waamaleki kwa sababu waliwapiga Waisraeli walipokuwa wanatoka Misri. Sasa, nenda ukawashambulie na kuangamiza vitu vyote walivyo navyo. Usiwaache hai, ila uwaue wote: Wanaume kwa wanawake, watoto wachanga na wanyonyao, ng'ombe, kondoo, ngamia na punda.’”
1 Samueli 15:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Samweli akamwambia Sauli, BWANA alinituma nikutie mafuta, uwe mfalme wa watu wake Israeli; basi sasa, isikilize sauti na maneno ya BWANA. BWANA wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu yale ambayo Waamaleki waliwatenda Waisraeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri. Basi sasa nenda ukawapige Waamaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyonavyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, na mtoto anyonyaye, ng'ombe na kondoo, ngamia na punda.
1 Samueli 15:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wakati huo Samweli akamwambia Sauli, BWANA alinipeleka nikutie mafuta, uwe mfalme wa watu wake Israeli; basi sasa, isikilize sauti na maneno ya BWANA. BWANA wa majeshi asema hivi, Nimeyatia moyoni mwangu mambo hayo Amaleki waliyowatenda Israeli, jinsi walivyowapinga njiani, hapo walipopanda kutoka Misri. Basi sasa enda ukawapige Amaleki, na kuviharibu kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala msiwaachilie; bali waueni, mwanamume na mwanamke, mtoto naye anyonyaye, ng’ombe na kondoo, ngamia na punda.
1 Samueli 15:1-3 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
Samweli akamwambia Sauli, “Mimi ndiye BWANA alinituma nikupake mafuta ili uwe mfalme juu ya watu wake Israeli; basi sasa sikiliza ujumbe kutoka kwa BWANA. Hili ndilo asemalo BWANA wa majeshi: ‘Nitawaadhibu Waamaleki kwa kile walichowatendea Israeli walipowavizia wakati walipanda kutoka Misri. Basi sasa nenda ukawashambulie Waamaleki na kuwaangamiza kabisa pamoja na kila kitu kilicho mali yao. Usiwahurumie; waue wanaume na wanawake, watoto na wale wanaonyonya, ngʼombe na kondoo, ngamia na punda.’ ”