Zaburi 50:7-11
Zaburi 50:7-11 BHN
“Sikilizeni watu wangu, ninachosema! Israeli, natoa ushahidi dhidi yako. Mimi ni Mungu! Mimi ni Mungu wako! Sikukaripii kwa sababu ya tambiko zako; hujaacha kunitolea tambiko za kuteketeza. Kwa kweli sina haja na fahali wa zizi lako, wala beberu wa mifugo yako; maana wanyama wote porini ni mali yangu, na maelfu ya wanyama milimani ni wangu. Ndege wote wa mwitu ni mali yangu, na viumbe vyote hai mashambani ni vyangu.


