Zaburi 50:7-11
Zaburi 50:7-11 Biblia Habari Njema (BHN)
“Sikilizeni watu wangu, ninachosema! Israeli, natoa ushahidi dhidi yako. Mimi ni Mungu! Mimi ni Mungu wako! Sikukaripii kwa sababu ya tambiko zako; hujaacha kunitolea tambiko za kuteketeza. Kwa kweli sina haja na fahali wa zizi lako, wala beberu wa mifugo yako; maana wanyama wote porini ni mali yangu, na maelfu ya wanyama milimani ni wangu. Ndege wote wa mwitu ni mali yangu, na viumbe vyote hai mashambani ni vyangu.
Zaburi 50:7-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Sikieni, enyi watu wangu, nami nitanena, Mimi nitakushuhudia, Israeli; Mimi ndimi niliye MUNGU, Mungu wako. Sitakukemea kwa ajili ya dhabihu zako, Na kafara zako ziko mbele zangu daima. Sitatwaa ng'ombe katika nyumba yako, Wala beberu katika mazizi yako. Maana kila mnyama-pori ni wangu, Na mifugo juu ya angani elfu. Nawajua ndege wote wa milima, Na wanyama wote wa mashamba ni wangu.
Zaburi 50:7-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Sikieni, enyi watu wangu, nami nitanena, Mimi nitakushuhudia, Israeli; Mimi ndimi niliye MUNGU, Mungu wako. Sitakukemea kwa ajili ya dhabihu zako, Na kafara zako ziko mbele zangu daima. Sitatwaa ng’ombe katika nyumba yako, Wala beberu katika mazizi yako. Maana kila hayawani ni wangu, Na makundi juu ya milima elfu. Nawajua ndege wote wa milima, Na wanyama wote wa mashamba ni wangu
Zaburi 50:7-11 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
“Sikieni, enyi watu wangu, nami nitasema, ee Israeli, nami nitashuhudia dhidi yenu: Mimi ndimi Mungu, Mungu wenu. Sikukemei kwa sababu ya dhabihu zako, au sadaka zako za kuteketezwa, ambazo daima ziko mbele zangu. Sina haja na fahali wa banda lako, au mbuzi wa zizi lako. Kwa maana kila mnyama wa msituni ni wangu, na pia makundi ya mifugo juu ya vilima elfu. Ninamjua kila ndege mlimani, nao viumbe wa kondeni ni wangu.