Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 12:1-8

Zaburi 12:1-8 BHN

Fanya haraka, ee Mwenyezi-Mungu! Watu wema wamekwisha; waaminifu wametoweka miongoni mwa watu. Kila mmoja humdanganya mwenzake, husema kwa kudanganya na kwa moyo wa unafiki. Ee Mwenyezi-Mungu uikomeshe hiyo midomo ya udanganyifu, na ndimi hizo zinazojigamba kupindukia. Wao husema: “Kwa ndimi zetu tutashinda; midomo tunayo, nani awezaye kututawala?” Lakini Mwenyezi-Mungu asema: “Kwa sababu maskini wanadhulumiwa, na wahitaji wanapiga kite, sasa naja, nami nitawapa usalama wanaoutazamia.” Neno la Mwenyezi-Mungu ni safi, safi kama fedha iliyosafishwa katika tanuri, naam, kama fedha iliyosafishwa mara saba. Utulinde, ee Mwenyezi-Mungu, utukinge daima na kizazi hiki kiovu. Waovu wanazunguka kila mahali; upotovu unatukuzwa kati ya watu.

Soma Zaburi 12