Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 12:1-8

Zaburi 12:1-8 SRUV

Tuokoe, ee BWANA, maana hamna tena amchaye Mungu Maana waaminifu wametoweka katika wanadamu. Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe, Wenye midomo ya kujipendekeza; Husemezana kwa mioyo ya unafiki; BWANA ataikata midomo yote ya kujipendekeza, Na ulimi unenao maneno ya kiburi; Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda; Midomo yetu ni yetu wenyewe, Ni nani aliye bwana juu yetu? Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya. Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba. Wewe, BWANA, ndiwe utakayetuhifadhi, Utatulinda na kizazi hiki milele. Wasio haki hutembea pande zote, Huku ufisadi ukitukuka kati ya wanadamu.

Soma Zaburi 12