Zaburi 12:1-8
Zaburi 12:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Fanya haraka, ee Mwenyezi-Mungu! Watu wema wamekwisha; waaminifu wametoweka miongoni mwa watu. Kila mmoja humdanganya mwenzake, husema kwa kudanganya na kwa moyo wa unafiki. Ee Mwenyezi-Mungu uikomeshe hiyo midomo ya udanganyifu, na ndimi hizo zinazojigamba kupindukia. Wao husema: “Kwa ndimi zetu tutashinda; midomo tunayo, nani awezaye kututawala?” Lakini Mwenyezi-Mungu asema: “Kwa sababu maskini wanadhulumiwa, na wahitaji wanapiga kite, sasa naja, nami nitawapa usalama wanaoutazamia.” Neno la Mwenyezi-Mungu ni safi, safi kama fedha iliyosafishwa katika tanuri, naam, kama fedha iliyosafishwa mara saba. Utulinde, ee Mwenyezi-Mungu, utukinge daima na kizazi hiki kiovu. Waovu wanazunguka kila mahali; upotovu unatukuzwa kati ya watu.
Zaburi 12:1-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tuokoe, ee BWANA, maana hamna tena amchaye Mungu Maana waaminifu wametoweka katika wanadamu. Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe, Wenye midomo ya kujipendekeza; Husemezana kwa mioyo ya unafiki; BWANA ataikata midomo yote ya kujipendekeza, Na ulimi unenao maneno ya kiburi; Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda; Midomo yetu ni yetu wenyewe, Ni nani aliye bwana juu yetu? Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya. Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba. Wewe, BWANA, ndiwe utakayetuhifadhi, Utatulinda na kizazi hiki milele. Wasio haki hutembea pande zote, Huku ufisadi ukitukuka kati ya wanadamu.
Zaburi 12:1-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA, uokoe, maana mcha Mungu amekoma, Maana waaminifu wametoweka katika wanadamu. Husemezana yasiyofaa kila mtu na mwenziwe, Wenye midomo ya kujipendekeza; Husemezana kwa mioyo ya unafiki; BWANA ataikata midomo yote ya kujipendekeza, Nao ulimi unenao maneno ya kiburi; Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda; Midomo yetu ni yetu wenyewe, Ni nani aliye bwana juu yetu? Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya. Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba. Wewe, BWANA, ndiwe utakayetuhifadhi, Utatulinda na kizazi hiki milele. Wasio haki hutembea pande zote, Ufisadi ukitukuka kati ya wanadamu.
Zaburi 12:1-8 Neno: Bibilia Takatifu 2025 (NENO)
BWANA tusaidie, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka; waaminifu wametoweka miongoni mwa wanadamu. Kila mmoja humwambia jirani yake uongo; midomo yao ya hila huzungumza kwa udanganyifu. BWANA na akatilie mbali midomo yote ya hila na kila ulimi uliojaa majivuno, ule unaosema, “Kwa ndimi zetu tutashinda; midomo ni mali yetu, bwana wetu ni nani?” “Kwa sababu wanyonge wanaonewa, na wahitaji wanalia kwa uchungu, nitainuka sasa,” asema BWANA. “Nitawalinda kutokana na wale wenye nia mbaya juu yao.” Maneno ya BWANA ni safi, kama fedha iliyosafishwa katika tanuru, iliyosafishwa mara saba. Ee BWANA, utatuweka salama na kutulinda na kizazi hiki milele. Watu waovu huenda wakiringa kila mahali wakati yule aliye mbaya sana ndiye anayeheshimiwa miongoni mwa watu.