Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 116:1-11

Zaburi 116:1-11 BHN

Nampenda Mwenyezi-Mungu, kwa maana anisikia, maana amesikia kilio cha ombi langu. Yeye amenitegea sikio, hivyo nitamwomba muda wote niishio. Hatari ya kifo ilinizunguka, vitisho vya kaburi vilinivamia; nilijawa na mahangaiko na majonzi. Kisha nikamlilia Mwenyezi-Mungu: “Ee Mwenyezi-Mungu, tafadhali unisalimishe!” Mwenyezi-Mungu amejaa wema na uaminifu; Mungu wetu ni mwenye huruma. Mwenyezi-Mungu huwalinda wanyofu; nilipokuwa nimekandamizwa aliniokoa. Uwe na utulivu mkuu, ee nafsi yangu, maana Mwenyezi-Mungu amenitendea mema. Ameniokoa kifoni na kufuta machozi yangu; akanilinda nisije nikaanguka. Nitatembea mbele yake Mwenyezi-Mungu, katika nchi ya watu walio hai. Nilikuwa na imani hata niliposema: “Mimi nimetaabika mno.” Hata nilisema kwa hofu yangu: “Binadamu wote hawaaminiki!”

Soma Zaburi 116