Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 116:1-11

Zaburi 116:1-11 NENO

Nampenda BWANA kwa maana amesikia sauti yangu; amesikia kilio changu ili anihurumie. Kwa sababu amenitegea sikio lake, nitamwita siku zote za maisha yangu. Kamba za mauti zilinizunguka, vitisho vya Kuzimu vilinipata, nikalemewa na taabu na huzuni. Ndipo nikaliitia jina la BWANA: “Ee BWANA, niokoe!” BWANA ni mwenye neema na haki, Mungu wetu ni mwingi wa huruma. BWANA huwalinda wanyenyekevu, nilipokuwa katika shida kubwa, aliniokoa. Ee nafsi yangu, tulia tena, kwa kuwa BWANA amekuwa mwema kwako. Kwa kuwa wewe, Ee BWANA, umeniokoa nafsi yangu na mauti, macho yangu kutokana na machozi, miguu yangu kutokana na kujikwaa, ili niweze kutembea mbele za BWANA, katika nchi ya walio hai. Nilimwamini BWANA, niliposema, “Mimi nimeteseka sana.” Katika taabu yangu nilisema, “Wanadamu wote ni waongo.”