Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 106:24-35

Zaburi 106:24-35 BHN

Kisha wakaidharau nchi ile ya kupendeza, kwa sababu hawakuwa na imani na ahadi ya Mungu. Walinungunika mahemani mwao, wala hawakumsikiliza Mwenyezi-Mungu. Hivyo Mungu akainua mkono akaapa kwamba atawaangamizia jangwani; atawatawanya wazawa wao kati ya watu, na kuwasambaza duniani kote. Kisha wakajiunga kumwabudu Baali kule Peori, wakala tambiko zilizotambikiwa mizimu. Waliichochea hasira ya Mwenyezi-Mungu kwa matendo yao, maradhi mabaya yakazuka kati yao. Lakini Finehasi akasimama kufanya malipizi, na yale maradhi yakakoma. Jambo hilo lakumbukwa kwa heshima yake, tangu wakati huo na nyakati zote. Walimkasirisha Mungu penye maji ya Meriba, Mose akapata taabu kwa ajili yao. Walimtia Mose uchungu rohoni, hata akasema maneno bila kufikiri. Hawakuwaua watu wa mataifa mengine kama Mwenyezi-Mungu alivyowaamuru. Bali walijumuika na watu wa mataifa, wakajifunza kutenda mambo yao.

Soma Zaburi 106