Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 106:24-35

Zab 106:24-35 SUV

Wakaidharau nchi ile ya kupendeza, Wala hawakuliamini neno lake. Bali wakanung’unika hemani mwao, Wala hawakuisikiliza sauti ya BWANA. Ndipo alipowainulia mkono wake, Ya kuwa atawaangamiza jangwani, Na kuwatawanya wazao wao kati ya mataifa, Na kuwatapanya katika nchi mbali. Wakajiambatiza na Baal-Peori, Wakazila dhabihu za wafu. Wakamkasirisha kwa matendo yao; Tauni ikawashambulia. Ndipo Finehasi akasimama akafanya hukumu; Tauni ikazuiliwa. Akahesabiwa kuwa ana haki Kizazi baada ya kizazi hata milele. Wakamghadhibisha penye maji ya Meriba, Hasara ikampata Musa kwa ajili yao, Kwa sababu waliiasi roho yake, Akasema yasiyofaa kwa midomo yake. Hawakuwaharibu watu wa nchi Kama BWANA alivyowaambia; Bali walijichanganya na mataifa, Wakajifunza matendo yao.

Soma Zab 106