Methali 29:15-17
Methali 29:15-17 BHN
Adhabu na maonyo huleta hekima, lakini mtoto aliyeachwa afanye apendavyo humwaibisha mama yake. Waovu wakitawala maovu huongezeka, lakini waadilifu watashuhudia kuanguka kwao. Mpe nidhamu mwanao naye hatakupa wasiwasi; yeye ataufurahisha moyo wako.