Methali 29:15-17
Methali 29:15-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Adhabu na maonyo huleta hekima, lakini mtoto aliyeachwa afanye apendavyo humwaibisha mama yake. Waovu wakitawala maovu huongezeka, lakini waadilifu watashuhudia kuanguka kwao. Mpe nidhamu mwanao naye hatakupa wasiwasi; yeye ataufurahisha moyo wako.
Shirikisha
Soma Methali 29Methali 29:15-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye. Waovu wakiongezeka, maasi huongezeka; Bali wenye haki watayatazama maanguko yao. Mrudi mwanao naye atakustarehesha; Naam, atakufurahisha nafsi yako.
Shirikisha
Soma Methali 29Methali 29:15-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye. Waovu wakiongezeka, maasi huongezeka; Bali wenye haki watayatazama maanguko yao. Mrudi mwanao naye atakustarehesha; Naam, atakufurahisha nafsi yako.
Shirikisha
Soma Methali 29