Methali 23:26-28
Methali 23:26-28 BHN
Mwanangu, nisikilize kwa makini, shikilia mwenendo wa maisha yangu. Malaya ni shimo refu la kutega watu; mwanamke mgeni ni kama kisima chembamba. Yeye hunyemelea kama mnyanganyi, husababisha wanaume wengi kukosa uaminifu.