Methali 20:1-4
Methali 20:1-4 BHN
Divai huleta dhihaka na kileo huleta ugomvi; yeyote anayevutiwa navyo hana hekima. Ghadhabu kali ya mfalme ni kama simba angurumaye; anayemkasirisha anayahatarisha maisha yake. Ni jambo la heshima kuepa ugomvi; wapumbavu ndio wanaogombana. Mvivu halimi wakati wa kulima; wakati wa mavuno atatafuta asipate chochote.