Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 20:1-4

Mithali 20:1-4 SRUV

Mvinyo hudhihaki, kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima. Utisho wa mfalme ni kama ngurumo ya simba; Amkasirishaye huitendea dhambi nafsi yake. Mtu kujitenga na ugomvi ni heshima kwake; Bali kila mpumbavu ataka kugombana. Mtu mvivu hataki kulima wakati wa baridi; Hivyo wakati wa mavuno ataomba, hana kitu.

Soma Mithali 20