Mithali 20:1-4
Mithali 20:1-4 NENO
Mvinyo ni mdhihaki na kileo ni mgomvi; yeyote apotoshwaye navyo hana hekima. Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba; yeye amkasirishaye hupoteza uhai wake. Ni kwa heshima ya mtu kujitenga ugomvi, bali kila mpumbavu ni mwepesi kugombana. Mvivu halimi kwa majira; kwa hiyo wakati wa mavuno hutazama lakini hapati chochote.